Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limetoa mafunzo kwa wajasiriamali kutoka vikundi vya wakina mama 88, vijana 36 pamoja na vikundi vya watu wenye ulemavu 36 kutoka katika Wilaya 5 za Jiji la Dar es Salaam.
Mikopo hiyo inatokana na asilimia 10 ya Mapato ya Ndani yanayokusanywa na Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam hutolewa kila mwaka kwa vikundi hivyo ili kuviwezesha kujikwamua kiuchumi, kujiongeza kipato na kupunguza tatizo la ajira kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza leo Desemba 24, 2020 wakati wa mafunzo hayo ya siku moja yaliondaliwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu Bi. Margareth Mazwile amesema mafunzo hayo ya siku moja kwa lengo la kuwajengea uwezo vikundi vya kina mama, vijana na watu wenye ulemavu.
“Tunatoa mafunzo haya kwa sababu tunatarajia kutoa mkopo kwa vikundi hivyo wenye thamani ya shilingi za Kitanzania milioni 547”, Amesema Mazwile.
Aidha, Mazwile amesema mafunzo hayo yatawasaidia wajasiriamali hao ili waweze kutumia mikopo hiyo ikiwemo jinsi ya kutumia mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa na kujua namna ya kutafuta masoko katika biashara zao, uandaaji wa mipango ya biashara, uwekaji wa kumbukumbu pamoja na kufahamu namna ya uwekaji wa akiba.
“Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwawezesha waweze kutumia mkopo huu vizuri katika kubuni miradi ambayo itakayowezesha kubadilisha maisha yao” Ameongeza kusema.
Katika hatua nyingine, Mazwile amewataka wajasiriamali hao kutumia fedha hizo kama walivyopanga ili waweze kurejesha mikopo na kutoa fursa kwa vikundi vingine kuweza kupata mikopo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.