Kamati ya Fedha na Utawala Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya Pili ya mwaka wa Fedha 2022/2023 (Oktoba-Desemba 2022) ambapo leo tar 16 Februari, 2023 imetembelea Vituo vya afya vya Mzinga, Gulukakwalala na Kiwalani pamoja na Shule ya Sekondari Minazi Mirefu.
Akizungumza kwenye ziara hiyo Mstahiki Meya wa Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Omary Kumbilamoto @meya_wa_jiji_dar amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kiasi cha Sh. Bil 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya vya Segerea, Kiwalani (Ujenzi wa jengo la Maabara,Wodi ya Wazazi, Upasuaji pamoja na jengo la Wagonjwa wa nje) na Gulukakwalala ambapo kila kimoja kilipokea kiasi cha shilingi Mil. 500. PiaHalmashauri hiyo imetenga kiasi cha Shilingi Mil. 68 kwa ajili kumalizia ujenzi wa Wodi ya Wazazi pamoja na Maabara katika Kituo cha Afya cha Gulukakwalala.
Aidha Mhe. Kumbilamoto ameongeza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mapato yake ya ndani ilitenga kiasi cha Bil.1.6 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mzinga cha ghorofa ambacho ujenzi wake unaendelea.
Naye, Mkuu wa Shule ya Sekondari Minazi Mirefu Mwl. Aveline Chugulu amesema Shule hiyo ipo katika kutekeleza mradi wa madarasa 20 ya ghorofa ambapo kutakuwa na madarasa 45 katika shule hiyo pindi ujenzi utakapokamilika. Mpaka sasa Shule hiyo imepokea kiasi cha Mil.220 kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mapato yake ya ndani.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo imewataka Wakandarasikumaliza Miradi ndani ya wakati uliopangwa huku ikitoa angalizokuchukuliwa hatua kwa Mkandarasi atakayechelewesha mradi kwani kukamilika kwa miradi hiyo kutawapunguzia Wananchi wa maeneo ya jirani adha ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma hizo za kijamii.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.