Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, amesema kuwa makusanyo ya mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yanaendelea kuwa chachu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, hususan katika sekta ya elimu.
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Februari 2026 alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa lenye lifti, madarasa 20 pamoja na matundu 45 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Kipunguni.
Mhe. Mpogolo amesema kuwa mafanikio hayo yanatokana na usimamizi madhubuti wa ukusanyaji wa mapato ya ndani, hali inayoiwezesha Halmashauri kuelekeza fedha katika miradi ya kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi. Ameongeza kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo utasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Akizungumzia mchango wa Serikali Kuu, Mpogolo amesema:
“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatamani kuona elimu ya Tanzania inapanda juu zaidi. Ndani ya Halmashauri yetu ameleta zaidi ya shilingi bilioni 36 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu, fedha ambazo zimewezesha ujenzi wa shule, madarasa ya ghorofa pamoja na miundombinu bora kwa wanafunzi wetu.”
Amesisitiza kuwa Halmashauri itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, sambamba na kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo endelevu ya Jiji.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.