Na: Shalua Mpanda
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ndugu Elihuruma Mabelya amesema wamejipanga kuhakikisha walimu wanapata maslahi yao yakiwemo madeni wanayodai kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo leo hii wakati akikagua uwekaji wa lifti katika jengo la ghorofa tano la shule ya sekondari ya kata Kipunguni.
Amesema uboreshaji wa miundombinu ya elimu unapaswa kwenda sambamba na mazingira mazuri na utulivu kwa walimu ili waweze kufundisha kwa ufanisi.
"Tunataka mwalimu akitoka nyumbani kazi yake ni moja tu, kazi yake ni kufundisha na kuzalisha wanafunzi bora na wenye uwezo bora na wenye msaada kwa Taifa". Alisema Mkurugenzi Mabelya.
Katika kufanikisha hilo, Mkurugenzi huyo wa Jiji amesema ameunda kamati ya kushughulikia madeni yote ya walimu ili walipwe madeni hayo.
Shule hiyo ya Kipunguni ni shule ya pili kuwa na miundombinu ya lifti katika jengo lake ikifuatiwa na shule ya sekondari Bonyokwa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.