• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Kamati ya kudhibiti UKIMWI Jiji la DSM yatembelea vituo vinavyojishughulisha na uelimishaji wa shughuli za kudhibiti UKIMWI

Tarehe iliyowekwa: February 16th, 2022

Na: Judith Damas

Wajumbe wa kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 16 Februari 2022,  wamefanya ziara ya kukagua vituo  vinavyojishughulisha na utekelezaji wa kudhibiti UKIMWI vilivyopo Kata ya Buguruni Jijini Dar es Salaam .


Kamati hiyo inayoongozwa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,  Mhe.Saady Khimji iliweza kutembelea vituo viwili vinavyojishughulisha katika kuimarisha Shughuli za kuthibiti UKIMWI ambovyo ni Kituo cha afya Buguruni ambacho kina kitengo cha huduma rafiki kwa vijana na Kamati ya kudhibiti UKIMWI Kata ambapo katika kituo cha afya Buguruni wameweza kupambana kudhibiti UKIMWI kwani wameweza kuanzisha huduma rafiki kwa vijana na pia wameweza kuanzisha kikundi cha Buguruni Youth Peer Educators (BUYOPE) ambacho hutumia sanaa mbalimbali kama ngoma pamoja na maigizo lengo likiwa ni kutoa elimu kwa vijana wengine juu Kujitambua na kujikinga  dhidi ya UKIMWI, ukatili wa kijinsia, elimu juu ya matumizi ya dawa za kulevya, elimu juu ya kutumia uzazi wa mpango pamoja na kujikinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Korona (COVID-19).


Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Saady Khimji ameweza kumpongeza Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Buguruni pamoja na timu nzima ya madaktari na wauguzi kwa kuweza kuanzisha huduma rafiki kwa vijana kiafya na kijamii ambapo huduma hii itawaleta karibu vijana wetu hivyo kuongeza nguvu kazi ya Taifa letu.


Mhe. Khimji amesema "Nawapongeza sana vijana wa Buguruni Youth Peer Educators (BUYOPE) kwa shughuli mnazozifanya za kuelimisha Jamii juu ya kulinda afya zao pia kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwaelimisha baadhi ya vijana wenye maambukizi ya UKIMWI lengo likiwa ni kuwasaidia, hivyo kwa vijana waliokwisha pata maambukizi ya virusi vya UKIMWI waweze kuunganishwa katika Konga ili kuweza kushirikiana na wengine katika kutekeleza shughuli za Konga."


Sambamba na hilo Mhe. Khimji ameeleza kua  kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam watahakikisha wanashirikiana na vikundi hivi kwa kuwawezesha vijana hawa kupata mkopo na pia watahakikisha kamati zote za kudhibiti UKIMWI ngazi ya Kata zina fanya kazi kikamilifu lengo likiwa ni      kuimarisha afya za wananchi hususani vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa na ambao ndio waathirika wakubwa wa majanga haya.


Naye Mratibu wa UKIMWI wa Halmashauri ya Jiji la DSM, Ndug. Barnabas Kisai ametoa shukrani zake kwa wajumbe wa Kamati ya UKIMWI ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaa na kuahidi ushirikiano katika kutekeleza yote aliyoagizwa kuyafanya ili kupunguza maambukizi ya usambaaji wa virusi vya UKIMWI na hatimaye kuongeza nguvu kazi ya Taifa.


Kwa upande wake Mratibu wa vijana Kituo cha afya Buguruni Sr. Janeth Nyera ameeleza kua huduma rafiki kwa vijana imeweza kuwa chachu kubwa kwa vijana kwani wameweza kuwaunganisha vijana wa makundi na rika mbalimbali wenye matatizo mbalimbali ya  kiafya na kijamii  ambao walikua na hofu ya kueleza matatizo yao kipindi cha nyuma hivyo kwa kushirikiana na vijana hao wameweza kuelimisha na kuwasaidia vijana wengi pia ameeleza kuwa vijana hao wameweza kutengewa siku yao maalumu ya kufika kituoni hapo ambayo ni siku ya Jumamosi hivyo ameahidi kushirikiana kikamilifu na Kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam  na amemtaka mwakilishi wa Konga kuweza kuwatembelea kila Jumamosi ili kukutana na vijana walio na maambukizi ya VVU lengo likiwa ni kuwaunganisha na konga na kuwaelimisha zaidi ili wasikate tamaa ya maisha.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.