Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Charles akiambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora J. Liana pamoja na wataalam kutoka OR-TAMISEMI leo tarehe 05 Septemba, 2017 amefanya kikao na wageni kutoka Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania wakiwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Miundominu na Mazingira ya nchini Uholanzi ili kujadili kwa pamoja namna bora ya usimamizi wa taka ngumu zinazozalishwa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Mstahiki Meya ameeleza kuwa usimamizi na uendelezaji wa shughuli za dampo la kutupia taka ngumu katika Jiji la Dar es Salaam unafanywa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika dampo lililopo katika eneo la Pugu Kinyamwezi katika Manispaa ya Ilala. Dampo hilo lina ukubwa wa hekta 65 ambao ni sawa na ekari 162.
Eneo hilo lilifanyiwa upembuzi yakinifu wa athari za mazingira, "Environmental Impact Assessment", na kuanza kutumika rasmi mwaka 2007 Halmashauri ya Jiji ilipokamilisha kuweka mipaka na kuweka miundombinu muhimu ya kufanikisha kazi ya kusafirisha taka kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji na kuzihifadhi katika eneo hilo.
Jiji la Dar es Salaam linakadiriwa kuzalisha taka ngumu tani 4,500 kwa siku na kati ya hizo wastani wa tani 1,200 hadi 1,800 zinazolewa na kutupwa kila siku katika dampo hilo ambazo ni sawa na asilimia 43 hadi asilimia 48.
Lengo la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni kujenga dampo la kisasa linalopaswa kukidhi matakwa yote ya kiafya na kimazingira, “Sanitary Landfill”. Uendeshaji wa madampo kwa teknolojia hii hutumika sehemu nyingi duniani hususan katika nchi zinazoendelea.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.