• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, Jiji la DSM lafanya maombi na dua ya kuliombea Taifa

Tarehe iliyowekwa: April 22nd, 2024

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 22, Aprili 2024 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanya Maombi na Dua ya kuliombea Taifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam yalioambatana na kaulimbiu isemayo “Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleao ya Taifa Letu.”

Akiongoza hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameeleza kuwa “Tumeandaa Maombi na Dua ya kuliombea Taifa letu ikiwa ni sehemu ya Kumshukuru Mungu kwa kufikisha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa amani kwani kama Taifa tumeshikamana na tumeimarika kwa miaka 60 hivyo hatuna budi kufanya Maombi na Dua kwaajili ya kuendelea kuimarisha amani ya nchi yetu.”

Sambamba na hilo Mhe. Mpogolo ameendelea kusema “Katika maombi na Dua hizi tunaendelea kumuombea Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuendelea kuimarisha Muungano kwa amani pamoja na kuhakikisha nchi yetu inaendelea kupata maendeleo bila kusahau kuombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaoenda kufanyika Oktoba 2024 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 ufanyike kwa Amani na tupate viongozi bora zaidi watakaoendelea kutuletea maendeleo.”

Kwa upande mwingine Mhe. Mpogolo amewahakikishia Wananchi wa Wilaya ya Ilala kutatua changamoto ya athari za mvua kwani tayari amewaelekeza wataalamu kutoka TARURA wakiambatana na Wahandisi kutoka Jiji la Dar es Salaam kutambua maeneo yote yaliyoathiriwa na mvua ili pindi mvua zitakapopungua maeneo hayo yafanyiwe marekebisho.

Aidha, kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Jomaary Satura ameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa dini kuliombea Taifa letu huku akiwahakikishia kushirikiana na watendaji wake kutatua kwa wakati changamoto zinazowakabili wananchi wa Wilaya ya Ilala kama Mheshimiwa Rais anavyoelekeza.

Akitoa Shukrani zake kwa viongozi wa Dini walioshiriki kuliombea Taifa, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto ameeleza kuwa “Kupitia Maombi na Dua hizi za kuliombea taifa kufikisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Imani yangu maombi haya yatadumisha Amani na yatakuwa chachu ya maendeleo kwa nchi yetu."

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Sheikh wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuandaa siku ya Maombi na Dua ya kuliombea Taifa kwaajili ya Muungano kwani maombi haya ni sehemu ya uzalendo pamoja na mshikamano kwa viongozi huku akiahidi kusimama na kuimarisha Muungano wa Tanzania kupitia Dua na Sala ili nchi iendelee kuwa na amani.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.