Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 1 Mei, 2017 wameungana na wafanyakazi wenzao duniani katika kusherekea Siku ya Wafanyakazi Duniani. Siku ya hii kwa Tanzania hujulikana kama Siku ya Wafanyakazi Duniani yaani Mei Mosi, inasherehekewa kila mwaka tarehe 1 Mei.
Sherehe za Mei Mosi kwa Jiji la Dar es Salaam mwaka 2017 zilianza kwa maandamano ya wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali za binafsi na umma kuanzia Ofisi za TUCTA Makao Makuu zilizopo Mnazi Mmoja kuelekea katika Uwanja wa Uhuru na kupokelewa na mgeni rasmi Mhe. Magreth Sitta (Mb).
Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka 2017 kitaifa yamefanyika katika uwanja wa mpira wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alipokea maandamano ya wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali nchini za binafsi na umma.
Kauli mbiu ya Mei Mosi mwaka 2017 inasema "UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE KULINDA HAKI NA HESHIMA YA WAFANYAKAZI". Kauli mbiu hii inazingatia utu wa wafanyakazi hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika mabadiliko makubwa ya uchumi wa viwanda dhana ambayo Tanzania ya viwanda inatuelekeza kuwa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.