Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo akiwa ameambatana na Viongozi wa Dini pamoja na viongozi mbalimbali wameshiriki Katika kongamano maalum la maombi na Dua kwa madereva wa bodaboda na bajaji, kuiombea Nchi ya Tanzania kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kongamano hilo Maalum lililoandaliwa na Shirikisho la vyama vya Madereva Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam (SHIVYAMAPIDA), Mkuu wa Wilaya hiyo amewasihi madereva bodaboda na bajaji Mkoa wa Dar es salaam kuunga mkono juhudi za serikali Katika kudumisha amani ya Nchi na kuongeza kuwa amani ya Nchi hulindwa na mwananchi mmoja mmoja huku akilitaja kundi hilo kuwa ni kundi muhimu Katika kulinda amani kutokana na aina ya kazi wanayoifanya.
Amesema Serikali itaendelea kuweka Mazingira wezeshi Kwa kundi hilo muhimu Katika uchumi wa Taifa, ikiwa ni pamoja na kuwawekea vituo vya kutosha ili kuwarahisishia majukumu yao ya kazi.
Kwa upande wao viongozi wa dini wakiongozwa na Jumuiya ya maridhiano na amani, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Walid Alhad Omar pamoja na Mtume Boniface Mwamposa, mbali na kuwapongeza viongozi wa shirikisho hilo Kwa kuandaa kongamano hilo la kumuombea Rais Samia na Nchi Kwa ujumla, wamewasisitiza kudumisha amani ya Nchi, na kujiepusha na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Naye mwenyekiti wa shirikisho hilo la vyama Vya bodaboda na bajaji Said Kagomba amewataka madereva bodaboda na bajaji kote Nchini kuzingatia misingi ya Sheria na taratibu zinazo waongoza kwenye utendaji wao wa kazi,ikiwa ni pamoja na kithamini kazi yao kwani ndio inayowaingizia kipato kwaajili ya kuendesha maisha yao na familia zao Kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.