Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua ukuta wa bahari wa mita 820 wenye lengo la kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuboresha maeneo ya fukwe kwa kuzuia mmomonyoko wa udongo katika kingo za bahari ya Hindi maeneo ya barabara ya Barack Obama (Ocean Road).
Uzindizi huo umefanyika katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Katika hotuba yake Mhe. Samia Suluhu amewataka wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kutunza miundombinu na mazingira ya eneo la ukuta ili kuwa nadhifu kwa ajili ya kupumzikia na kukuza utalii jijini.
Kaulimbiu ya kitaifa inayoongoza maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa mwaka 2018 ni “Mkaa Gharama; Tumia Nishati Mbadala”. Kaulimbiu hii inahimiza jamii kupunguza matumizi makubwa ya nishati ya mkaa ambayo yamesababisha kiasi kikubwa cha misitu yetu kuteketezwa.
Mama Samia Suluhu amehitimisha hotuba yake kwa kuwataka Watanzania kuelewa athari za ukataji wa miti kiholela na kuhakikisha wanakuwa walinzi wa kwanza wa mazingira.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.