Na: Shalua Mpanda
Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa ufungaji wa taa 213 za solar kampuni ya M/S EH Enginerring Company Ltd wametakiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda wa siku 60 kama masharti ya mkataba yanavyoelekeza.
Wito huo umetolewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto mara baada ya utiaji saini wa Mkataba huo kati ya Halmashauri ya Jiji na Kampuni hiyo Disemba 28, 2024.
Mhe. Kumbilamoto amesema wananchi wanatamani kuona miradi inakamilika kwa wakati ili waweze kufurahia kodi zao wanazolipa.
"Niwatake Wakandarasi mliopata nafasi hii mkamilishe mradi huu kwa wakati na lazima mtuambue kuwa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatoa fedha nyingi kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora". Alisisitiza Kumbilamoto
Aidha, Meya huyo amemsifu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kuweza kuvunja mikataba zaidi ya 9 ya wakandarasi walioshinda kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
"Nikwambie tu Mkuu wa Wilaya, sisi madiwani hapo nyuma tulikuwa tunakwamishwa sana na wakandarasi kwa kutokamilisha miradi mingi kwa visingizio tu,ila toka Mkurugenzi huyu amefika hapa ameshavunja mikataba 10 na sasa miradi mingi inaendelea vizuri".Aliongeza Meya huyo
Jumla ya taa 213 zenye thamani ya milioni 818,833,152 zinatarajiwa kufungwa katika maeneo ya mitaa ya Mafia, Tandamti, Pemba, Lumumba na Magogoni huku nyingine zikifungwa kituo cha mabasi Stesheni, mnada wa mifugo Pugu, Hospitali ya Wilaya Kivule na eneo la Vingunguti ndani ya miezi miwili kuanzia siku ya utiaji saini wa Mkataba huo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.