Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 01 Julai, 2017 wamefanya Mkutano wa Baraza la kawaida la robo ya tatu na kupitisha mihtasari ya Kamati pamoja na taarifa mbalimbali za Kamati za Kudumu za Halmashauri ya Jiji ambazo ni; Kamati ya Fedha na Uongozi, Mipango na Uratibu, Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu, Huduma za Jamii, na Kamati ya Maadili iliyofanyika katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2017.
Wenyeviti wa Kamati husika waliwasilisha taarifa za Kamati zao na Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walizipokea, kuzijadili na kuzipitisha ili zibaki kuwa kumbukumbu sahihi kwa Halmashauri.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam ametoa pongezi kwa Wajumbe wa Baraza la Madiwani na timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kufanikisha utekelezaji wa mipango ya miradi ya maendeleo na kuendelea kusisitiza kwamba mipango mbalimbali ya kukuza, kuhifadhi na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo jijini kwa kutumia Kituo cha Urithi wa Ubunifu wa Majengo na Utalii kilichopo katika jengo la Old Boma itekelezwe mapema ili kuwa chanzo cha mapato katika Jiji letu.
Mkutano huo wa Baraza la Madiwani umehudhuriwa na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wamepata fursa ya kusikiliza taarifa mbalimbali za mipango ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.