Katika kusherehekea sherehe za Miaka 58 ya Muungano ambazo hufanyika kila mwaka ifikapo Aprili 26 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla ameshiriki zoezi la usafi katika sehemu za kutolea huduma za afya ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam usafi huo umefanyika katika hospital ya taifa ya Muhimbili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe hizo.
Zoezi hilo la usafi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa DSM Mhe. Amos Makalla liliweza kuhudhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Watumishi kutoka Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Wadau mbalimbali wakiwemo bank ya NMB, Wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania na Zanaki pamoja na wanachi wengine wakiongozwa na vijana wa bodaboda waliofika kwa lengo la uchangiaji damu katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika zoezi hilo Mhe.Makalla amewahimiza watu kushiriki nae katika zoezi hilo la usafi katika zahanati na vituo vya afya vinavyowazunguka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Muungano."Nawapongeza sana wote mlioamka asubui na mapema na kujumuika nami katika zoezi hili la usafi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupendezesha na kusafisha Dar es Salaam niliyoizindua mwaka jana lengo likiwa ni kutunza mazingira na kuyaweka katika hali ya usafi."
Kwa upande mwingine Mhe. Makalla aliweza kuongoza zoezi la uchangiaji damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amewahamasisha wananchi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wengine pia aliweza kuwapongeza vijana wa bodaboda ambao wameweza kufika kwa wingi katika hospitali hiyo na kuweza kuchangia damu pamoja na kuchanja chanjo ya COVID-19 pamoja na kutoa wito kwa wananchi wengine kujijengea utaratibu wa kuchangia damu kwaajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndug. Ngw'ilabuzu Ludigija aliweza kutoa shukrani zake za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM kwa kuongoza zoezi zima la usafi hivyo kuwahimiza wananchi kijitokeza siku ya Jumamosi ya tarehe 30 April,2022 kufanya usafi ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya 'Safisha, Pendezesha Dar es Salaam' ambapo kimkoa mwezi huu itafanyika Wilaya ya Ilala.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.