Katika kuboresha Mazingira ya wafanyabiashara wa Nyama katika machinjio ya Vingunguti , Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija ametoa siku 30 Kwa wafanyabiashara hao kutumia Eneo la mabucha mapya ya Nyama bila malipo yoyote ili wajipange Vizuri katika kipindi hiki wanachohamia hapo Kutoka kwenye eneo la zamani.
Mkuu huyo ameyasema hayo alipotembelea Eneo la Mabucha mapya kujiridhisha na Juu ya Utekelezaji wa Maelekezo yake aliyotoa siku za hivi karibuni ya kuwataka wafanyabiashara wote wa Nyama katika machinjio ya Vingunguti Kuhamia katika Mabucha hayo yaliyojengwa na halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
"Kwa wale ambao hawajatekeleza nasisitiza kwamba Nyama ya mbuzi na Ng'ombe inayochinjwa Kwenye machinjio yetu ya Vingunguti ni Lazima iuzwe kwenye Mabucha haya ambapo ni mahali safi na Salama
Nafahamu eneo hili ni finyu Ndio maana nimemuelekeza Mkurugenzi Kuhakikisha analipa fidia Kwa nyumba za pembeni ili tuongeze Kujenga Mabucha Mengine lakini sitaki kuona biashara ya Nyama inafanyika kwenye mazingira machafu na wote wanaokaidi maagizo yangu watachukuliwa hatua za kisheria" Alisema Mh.Ludigija
Vile vile Mkuu wa Wilaya Amesema kuwa Serikali ya Rais Samia iweweka Fedha kwenye Ujenzi wa barabara ya Vingunguti Ili kurahisisha usafirishaji wa Nyama kimataifa pamoja na mikoa mingine ya hapa nchini hivyo ni Vyema wafanyabiashara hao wakubali mabadiliko na Sio kuishi Kwa Mazoea.
Kwa Upande wao wafanyabiashara wa Nyama wamepongeza hatua ya Serikali kuwajengea mabucha hayo ya kisasa na licha ya Kujitokeza Changamoto kadhaa ambazo tayari baadhi zimeshafanyiwa kazi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.