Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ngwilabuzu Ludigija leo tarehe 2 Disemba 2022 akiwa pamoja na mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndg. Saidi Side na Kamati ya Siasa wamefanya zoezi la upandaji wa miti katika maeneo ya Gereza la Segerea na Ukonga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru kila Wilaya iadhimishe kwa kufanya mambo mbalimbali na kuelezea mafanikio ambayo Wilaya husika wameyafikia.
Kuelekea siku hiyo Mhe. Ludigija amesema "Kilele cha Siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania yatafanyika Tarehe 9 Disemba 2022 na sisi kama Wilaya tutafanya mdaharo wa kujadili mafanikio ambayo wilaya yetu imeyafikia toka Nchi yetu ipate uhuru.
Kwa wilaya ya Ilala inampango wa kufanya shughuli nyingi za kijamii ambazo zitaleta tija kwa wananchi na jamii kwa ujumla ikiwemo usafi, mazingira, na kila idara yetu itafanya jambo ambalo kwa pamoja litafanikisha zoezi hili na malengo yetu mwaka 2022 ni kupanda miti Milioni 1 na laki tano (Milioni 1.5) na tayari maeneo mengi miti imepandwa.
Leo tumekuja hapa na kamati ya siasa ya Ilala lengo letu kubwa kuelekea maadhimisho ya sherehe za Maadhisho ya Uhuru kufanya kazi za kijamii ikiwemo kupanda Miti naomba wananchi watuunge mkono katika zoezi hili la upandaji wa miti ili kulinda mazingira pamoja na miti hii pia ni chanzo cha Mvua" alimalizia Mhe. Ludigija
Pia mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala Ndugu Saidi Side ambaye akiambatanana kamati ya siasa ya wilaya amesema "Nafarijika na kuwapongeza magereza ya Segerea na Ukonga kwa kutupatia nafasi hii muhimu ya kupanda miti katika maeneo haya,hii miti ikiwa yakutosha itafanya maboresho kutokana na msongamano wa watu maeneo yetu ya Wilaya ya Ilala watu wanahitaji hewa safi eneo letu lina Msitu wa Nyuki lakini upandaji huu wa miti utaenda kutekeleza hilo"
Kamati ya Siasa ikiwa katika kutekeleza agizo hili na kuweza kutembelea maeneo mengine mbalimbali ili kujionea utekelezwaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika wilaya ya Ilala kuangalia namna kazi na miradi mbalimbali inatekelezwa kwa ufanisi.
Mratibu Mwandamizi wa Magereza, Gereza la Mahabusu Segerea Hamisi Lisu amesema "Tunashukuru sana ujio wenu kwa kuchagua eneo hili kuwa eneo moja wapo la maadhimisho kwa upandaji wa Miti tunawaahidi miti hii tutaitunza na kuikuza tunawakaribisha tena siku nyingine kuja kuona miti hii".
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.