Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Mei 30, 2024 amefanya mkutano wa hadhara kwenye Jimbo la Segerea wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa jimbo hilo.
Akisikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo, RC Chalamila amepokea changamoto za masoko, miundombinu, migogoro ya Ardhi na kuzitatua papo kwa papo na nyingine kuzipatia utatuzi kwa kuwataka watendaji washughulikie mara moja.
Akiongea na wananchi, Mhe. Chalamila amewataka wananchi kuwa na uvumilivu pale ambapo Serikali inapambana kutatua tatizo la barabara .
“Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mapato yake ya ndani imetoa Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Kimanga kwa urefu wa Mita 400, kujenga mitaro ya kisasa kwa ajili ya kupitishia maji na kuweka taa za barabarani. Pia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mradi wa DMDP wanatarajia kutengeneza Barabara hii kwa urefu wa mita 700. Hivyo nawaomba sana wananchi wa kata hii ya kimanga kuwa wavumilivu hadi pale barabara itakapokamilika."
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutenga muda wa siku tatu katika Wilaya ya Ilala kwa kukagua miradi ya maendeleo pia kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Amesema “Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha Bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya ghorofa. Pia kutujengea kituo cha afya na kutuletea vifaa tiba. Hata hivyo nikuhakikishie sisi viongozi kwa kushirikiana na watendaji wa Halmshauri, kufanya kazi za bidii, kusimamia vyema mapato na zaidi kusimamia uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa haki na usawa."
Katika ziara hiyo Mhe. Chalamila aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala , wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Viongozi wa Chama wa Wilaya ya Ilala, Wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wengine kutoka Taasisi zinazowahudumia wananchi kwa ukaribu ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mji (TARURA) , Wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) pamoja na wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.