• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

RC Makalla ashiriki zoezi la usafi wa jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba

Tarehe iliyowekwa: September 24th, 2022

Na: Judith Damas na Amanzi Kimonjo.

 Katika kuendeleza  Kampeni ya Usafi "safisha,pendezesha Dar es Salaam" Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makalla  leo tarehe 24 Septemba, 2022 ameshiriki zoezi la usafi katika kata ya Mnazi Mmoja ambapo usafi huo hufanywa kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi.

Zoezi hilo la usafi lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam liliwahusisha Mkuu Wilaya ya Ilala,Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam ,Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam,madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,madiwani wa Manispaa ya Morogoro, Jeshi la Zimamoto, Watendaji kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Asasi mbalimbali ikiwemo ‘Juza Waste Pickere Initiative’  pamoja na wananchi wakiongozwa na vijana wa usafi kutoka Kajenjere  Trading  Company Limited.

Akizungumza katika zoezi hilo Mheshimiwa Amos Makalla amewata Wananchi kushiriki usafi kama desturi yao na sio kusubiri mpaka mwisho wa mwezi ufike ili kuweka mazingira safi na kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linapendeza na kuwa safi, "Nawapongeza wananchi wa Dar es salaam kwa kujitokeza na kushirikiana kufanya usafi,usafi ni afya kupitia usafi huu tutajikinga na  magonjwamengi ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu." 

Aidha Jiji la Dar es salaam limekua na mvuto sana kutokana na kampeni hii na kwa sasa Mkoa huu ni wa mfano kwa Mikoa mingine katika kuhamasika kufanya hivi kwani leo tuna wageni ambao ni madiwani kutoka Manispaa ya Morogoro ambao wameweza kushiriki nasi katika zoezi la usafi hii ni jinsi gani Mikoa mingine imeweza kuuunga mkono zoezi la usafi lengo likiwa ni kuiweka nchi yetu ya  Tanzania katika hali ya usafi.

"Sambamba na hilo pia Mheshimiwa  Makalla amezindua magari mawili yatakayotumika kukusanya taka maeneo mbalimbali ndani ya Jiji la Dar es salaam,magari hayo yaliyo chini ya kampuni ya usafi inayotambulika kwa jina la Kajenjere trading company hivyo uwepo wa magari hayo utaimarisha usafi katika Jiji letu na Mkoa mzima wa Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Ngw'ilabuzu Ludigija amewata Wananchi kushiriki usafi kama desturi yao na sio kusubiri mpaka mwisho wa mwezi ufike ili kuweka mazingira safi na kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linapendeza na kuwa safi, "Tuhakikishe kwamba usafi ni jambo la kwanza katika Wilaya yetu na ukilinganisha kwamba sisi ni Jiji Lazima tuendane na hadhi ya Jiji letu hivyo nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa kampuni zote zinazojihusisha na ukusanyaji wa taka ikiwemo Kajenjere Trading Company Limited kwani wanafanya kazi nzuri ya kuliweka Jiji letu katika hali ya  usafi".

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.