Katika kuadhimisha Siku ya Usafi Duniani Leo Septemba 21. 2024 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na viongozi wa Mazingira kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA) wamefanya usafi katika fukwe za Sea View lengo likiwa ni kuendana na kauli mbiu isemayo “Uhai Hauna Mbadala zingatia Usafi wa Mazingira” pamoja na kuhakikisha mazingira ya Jiji yanakua katika hali ya usafi.
Aidha, wakati wa zoezi hilo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini TPA imetoa Vifaa mbalimbali vya Usafi vitakavyotumika katika kusafisha na kutunza mazingira ya Fukwe za Sea view zilizopo Jijini Dar es salaam
Akikabidhi Vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Mazingira kutoka TPA Bw. Thobias Sonda amesema lengo la kugawa vifaa hivyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuweka Nchi katika Mazingira safi na salama.
Bw. Sonda amesema eneo la Fukwe hizo ni muhimu kwa sababu yanatembelewa na Watu mbalimbali kutoka maeneo tofauti kuja kupumzika
"Hivi Vifaa TPA imevikabidhi ili kuhakikisha maeneo haya yote yanakuwa safi na salama hivyo tunaimani na Serikali ya Mtaa huu itakuwa inaendelea na Zoezi la kufanya usafi Kila ifikapo tarehe ya mwisho wa mwezi". amesema.
Wakati huo huo, amewataka wadau mbalimbali wa Mazingira kufanya kazi kwa pamoja ili kuweka Fukwe hizo safi na salama zaidi
Nae Mwenyekiti wa Mtaa wa Seaview Victor Muneni ameishukuru TPA kwa kuwakabidhi Vifaa hivyo ambavyo vitawawezesha kuweka Mazingira safi na salama ya Fukwe hizo.
"Hapo awali tulikua tukikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Vifaa hivyo mara baada ya TPA kutukabidhi hivi Vifaa tutahakikisha Fukwe zetu zinakuwa safi na salama."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.