Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeshiriki kikamilifu katika maonesho ya sikukuu ya Wakulima Katika kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro na Dar es Salaam yanayofanyika katika mkoa wa Morogoro , Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere kuanzia tarehe 1-8 Agosti kila mwaka.
Katika Maonesho ya mwaka 2023 kaulimbiu ni Vijana na Wanawake ni Msingi Imara ya Mifumo Endelevu ya Chakula.
Katika Banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limetembelewa na viongozi pamoja na wananchi wanaotoka katika maeneo mbalimbali, wakionesha kufurahishwa na kujifunza teknolojia zilizosheheni ubunifu na kuleta tija katika uzalishaji.
Tukianza na Sekta ya Kilimo wameweza kujifunza teknolojia mbalimbali zikiwa ni pamoja naKilimo cha utengenezaji wa ustani za nyumbani , Kilimo cha uyoga na mapishi ya uyoga, kilimo cha bila kutumia udongo, Umwagiliaji kwa njia ya matone, kilimo cha mbogamboga kwa kutumia Kitalunyumba, uzalishaji wa miche bora ya matunda pamoja na kilimo cha mjini.
Aidha katika Mifugo wameweza kujifunza teknolojia kama Ufugaji wa kuku chotara, ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa, Usindikaji wa maziwa, Ufugaji wa Bata bukini, Kuku wa Asili, Ufugaji wa Mbwa , uzalishaji wa malisho ya mifugo pamoja na upimaji wa ubora wa maziwa.
Hali Kadhalika katika Uvuvi wameweza kujifunza Ufugaji Samaki kwenye Tenki, Upimaji wa ubora wa mabwawa, Utotoleshaji vifaranga vya samaki, utengenezaji wa chakula cha samaki, Ufugaji wa Samaki kwenye bwawa lisilo la kuchibwa pamoja na Usindikaji mazao ya Uvuvi.
Aidha Halmashauri ya Jiji la Da es Salaam imetekeleza kwa vitendo sera ya kila Halamshauri kutenga asilimia 10% ya mapato yake ya ndani kutoa mikopo kwa Wanawake Vijana, na watu wenye ulemavu ambapo katika banda la Jiji Wajasiriamali waliowezeshwa kupitia 10% wamepewa fursa ya kuonesha bidhaa walizozitengeneza na mazao yatokanayo na kilimo na mifugo kwa kuongeza thamani ikiwa ni pamoja na bidhaa za usindikaji kama viungo vya chakula, Unga lishe, Maziwa, mvinyo na asali bidhaa zinazotokana na zao la ngozi kama mikoba, viatu,mikanda pamoja kofia.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.