Na: Shalua Mpanda
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo amesema wao kama viongozi wanatekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati wa uzinduzi wa treni ya Mwendokasi (SGR) la kuwataka kukamilisha miradi inayowagusa wananchi moja kwa moja.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo leo Januari 15, 2025 wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa umaliziaji wa jengo la ghorofa la shule ya sekondari Kipunguni.
"Tunaposema Serikali imedhamiria kutimiza yale inayoahidi,mfano ni ukamilishwaji wa jengo la shule hii ambao ni utekelezaji wa agizo la Rais alilotoa kwamba tuhakikishe miradi inakamilika". Alisema Mkuu huyo wa Wilaya
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imedhamiria kukamilisha miradi yote iliyokwama kutokana na sababu mbalimbali na ukamilishaji huu wa miradi una lengo la kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo huduma za afya, elimu nk.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.