Umoja wa Wajasiriamali Walemavu Mkoa wa Dar es Salaam (UWAWADA) leo Machi 17, 2023 wamefanya kongamano la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi wake na kumshukuru kwa kuendelea kusisitiza mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ambayo watu wenye ulemavu ni wanufaika.
Akizungumza kwenye kongamano hilo lililofanyika kwenye Viwanja vya Karume kwa niaba ya Mkuuwa Mkoa wa Dar es Salaam, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Selemani alitoa pongezi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza Miradi yote iliyoachwa na Hayati John Pombe Magufuli kwa kasi na ubora uleule, na kumshukuru kwa kuendelea kusisitiza mikopo inayotolewa kwa watu wenye ulemavu kwani huwasaidia kuwainua kiuchumi.
Aidha Bi. Charangwa amewapongeza Umoja wa Wajasiriamali Walemavu Dar es Salaam (UWAWADA) “Niwapongeze kwa kuandaa shughuli nzuri yenye lengo zuri la kumpongeza mama yetu, mnaonesha jinsi gani mna shukurani maana kila mtu angeweza kukaa peke yake na kushukuru, hivyo mtaenda kumtia Mhe. Rais” Amesema Bi. Charangwa.
Nae Ndg. Juma Malecha ambae ni Mwenyekiti wa Umoja huo amesema wanashukuru Uongozi bora wa Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu kwani ndani ya miaka miwili ya uongozi wake aliweza kukutana na Watu wenye Ulemavu na kusikiliza changamoto zao, Pia Mhe. Rais ameendelea kusisitiza suala la mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri huku kundi hilo likiwa miongoni mwa makundi yaliyonufaika na mikopo hiyo kwa asilimia 2. Aliongeza kwa kusema kuwa ndani miaka miwili hiyo Mhe. Dkt. Samia ameweza kufufua Vyuo vya Ufundi kwa Watu wenye Ulemavu ambavyo vilikuwa vimefungwa ambapo katika vyuo hivyo wanapata chakula na malazi bure na pia amekemea unyanyapaa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.