Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Rais Magufuli ameeleza kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa itarahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria na kukuza biashara na nchi za jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na kukuza uchumi nchini katika njanja za madini, utalii, kilimo sambamba na kurahisisha usafirishaji wa malighafi.
Mhe. Rais pia amezitaja faida za reli hiyo ya kisasa kuwa ni pamoja kusaidia kutunza barabara nchini kwani malighafi na mizigo mbalimbali itasafirishwa kupitia reli hiyo na kuziacha barabara bila ya magari mengi na hivyo kudumu kwa kipindi kirefu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.