Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Selemani leo tarehe 04 Aprili, 2023 amefanya kikao na wadau pamoja na wawekezaji mbalimbali kujadili namna ya kuweza kupanda Miti ya aina ya Mitende (Palm Tree) pembezeni mwa barabra ya kutoka airport mpaka Ikulu, kwa lengo la kujenga mandhari bora na inayovutia ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya “Safisha Pendezesha Dar es Salaam”
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa kihistoria Karimjee uliopo Posta Jijini Dar es Salaam kilikua na lengo la kuwakutanisha wadau na wafanyabiashara wote wanaofanya biashara kutoka eneo la airport mpaka Ikulu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya ‘Safisha Pendezesha Dar Es Salaam’ sambamba na kuwaomba waweze kupanda miti ya aina ya mitende (Palm Tree) pembezoni mwa barabara hiyo.
Akiongea katika kikao hicho Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi.Charangwa Selemani ameeleza kuwa “ Mazingira ndio sura bora kwa kila nchi pamoja Miji huu ndio msukumo mkubwa ambao Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla kuweza kuanzisha kampeni inayohamasisha na kuhimiza suala zima la kuweka Jiji katika hali ya usafi”
Sambamba na hilo Bi. Charangwa ameendelea kusema “Barabara ya Nyerere maarufu kama ‘smart road’ kwani hii ndio sura kwa wageni wote wanaoingia Nchini,hivyo inabidi tuweke mazingira yetu safi ili Jiji letu la Dar es Salaam lionekane katika Mvuto na muonekano ambao utakuwa ni wa kuvutia”.
Kwa upande wake Mdau kutoka SBS Bw. Alexanda Nyirenda ambaye ni mkuu wa uhusiano wa kiwanda cha SBC wanaojishughulisha na uzalishaji wa vinywaji baridi vya pespsi amesema mpango ni kitu kizuri sanaa kwani mazingira ni kitu bora kama mkuu wa Mkoa anavyohitaji hivyo kwa niaba ya wadau na wafanyabiashara wenzangu sisi tupo tayari kuunga mkono na kushirikiana na Mkuu wa Mkoa kuupendezesha Mkoa huu kwa kuweza kuboresha barabara ya mwalimu nyerere”
Vile vile, Bw. Salimu Kanji kutoka kampuni ya “Satani Coperative Limited” inayojishughulisha na uuzaji wa magari amesema “Tumeitikia wito na tumekubali kushirikiana na kutekeleza yote yanayohitajika kwa kupendezesha barabara kwa kupanda miti ya Mitende (Palm Tree)”.
Naye Mkuu wa kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Theresia Dennis amesema “Eneo hili la barabara ya kutoka airport mpaka Ikulu ni muhimu sana kwani viongozi pamoja na wageni kutoka nje ya nchi hutumia barabara hii hivyo lazima tuhakikishe tunapendezesha barabara hii kwa kuona umuhimu huo na kufanikisha hili tumeweza kuwahusisha wadau ili kuweza kufikia hatua bora ya utekelezaji”.
Mpango huu umeazimiwa kutekelezwa hivi punde baada ya kukamilisha mipango pamoja na taratibu ambazo kwa asilimia kubwa zinaenda kufikiwa malengo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.