Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam amewaongoza Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na timu ya Menejiment leo tarehe 06 Machi, 2018 katika ziara ya ukaguzi wa miradi inayoendelea ndani ya dampo la Pugu Kinyamwezi.
Wajumbe hao wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya kuingia dampo inayojengwa kwa kiwango cha zege yenye urefu wa kilometa 0.7 ili kuhakikisha barabara hiyo inapitika kipindi chote cha mwaka.
Katika hatua nyingine Wajumbe hao wameweza kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa ukuta kwa awamu ya nne wenye urefu wa mita 850 katika eneo la dampo ikiwa na lengo kuzuia taka mbalimbali zinazohifadhiwa zisifike kwenye makazi ya wananchi, kuliweka dampo katika ulinzi na kulinda mipaka dhidi ya wavamizi wa ardhi.
Aidha, Wajumbe hao wa Kamati za Fedha na Uongozi, Mipango na Uratibu, Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji pamoja na Kamati ya Maadili walipata fursa ya kutembelea mradi wa maji ambao umefanikiwa kutatua kero kubwa ya maji kwa wakazi wa eneo linalozunguka dampo la Pugu Kinyamwezi.
Wananchi wa eneo hilo wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Pugu, Mhe. Bonventure Mphuru na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mustafa, Bi. Bahati Omari wametoa shukrani zao za dhati kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuwawekea mradi huo wa maji.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.