• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Wakuu wa Shule za Sekondari Jiji la DSM waaswa kuongoza kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu

Tarehe iliyowekwa: August 31st, 2021

Na; Judith Msuya.

Wakuu wa Shule za Sekondari za Umma pamoja na za Binafsi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Augusti 21, 2021 wamefanya kikao kazi kwa ajili ya maandalilizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2022, kikao hicho  kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Shaabani Robert Jijini Dar es Salaam kimehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Maafisa Elimu kata pamoja na mafundi ujenzi wanaotumika kujenga Shule mbalimbali.

Akizungumza katika kikao kazi hicho Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amesema kuwa wanafunzi takribani 28,480 wanatarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu ambapo makadirio ya wanafunzi watakao faulu wanatarajiwa kuwa Wanafunzi 26,800 ambao ni idadi kubwa na wanatakiwa kuingia darasani kwa wakati hivyo maandalizi lazima yafanyike mapema ili ifikapo Januari 2022 Wanafunzi wote watakaofaulu waweze kuingia darasani kwa wakati.

"Tumetenga fedha takribani milioni 900 kwaajili ya kuongeza madarasa na kununua vifaa vya shule Kwa baadhi ya Shule kwa ajili ya Wanafunzi watakao faulu kuingia kidato cha kwanza 2022 hivyo fedha hizo zitatolewa mapema ili taratibu za utekelezaji zianze kusudi tuweze kuepusha usumbufu uliojitokeza mwaka 2021 ambapo Wanafunzi walichelewa kuanza masomo kwa wakati muafaka kutokana na ujenzi kuchelewa kukamilika". alisema Mhe. Ludigija.

Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya amewasisitiza Wakuu wa Shule hao kuhakikisha wanatunza  nyaraka zote za malipo ya Miradi, barua za vikao pamoja na nyaraka zote za muhtasari wa vikao vyao zinahifadhiwa vizuri kwa ajili ya kumbukumbu za badaye bila kusahau kuwashirikisha wananchi wanaowazunguka kwani pamoja na kwamba fedha zinatolewa na Serikali lakini miradi hiyo inawahusu Wananchi hivyo sibudi kuwashirikisha Wananchi hao ili kufanya mambo kuwa mepesi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya ujenzi wa shule.

Kwa upande mwingine Mhe. Ludigija aliwapongeza Wakuu wa Shule kwa ushirikiano mzuri baina yao na viongozi wao kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021 kwa kujenga madarasa takribani 178 kwa muda mfupi  na hivyo kuwaagiza Wakuu wa shule kuhakikisha kuwa kuelekea kipindi hiki cha mitihani wahakikishe wanafunzi wote wamesajiliwa kama inavyotakiwa ili kuepusha usumbufu unaojitokeza kwa wanafunzi na Wazazi katika kipindi cha mitihani.

"Nawashukuru sana kwa mchango wenu na nawaahidi kushirikiana na nyinyi katika utekelezaji wa miundombinu, kudumisha michezo, nidhamu pamoja na taaluma katika shule zetu ili kuhakikisha Halmashauri yetu ya Jiji la Dar es Salaam inakua kinara katika kuboresha Elimu na Pia niwaombe 'local Fundi' unapopata kazi kwenye Jiji la Dar es Salaam unaikamilisha kwa wakati ili kuepusha usumbufu kwa Walimu wakuu wa Shule ambao wanasimamia Taaluma kwa watoto wetu."

Kikao kazi hicho kilicho funguliwa na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Ndug.Abdul Maulid ambaye amewasisitiza Wakuu wa Shule za Sekondari za Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam  kuhakikisha wanasimamia shule katika misingi ya kisheria, taratibu na kanuni katika kusimamia nidhamu ya Shule, usafi wa mazingira, ulinzi na usalama, michezo na burudani  pamoja na kuhakikisha wanasimamia vyema miundombinu ya Shule ili kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali kwenye 'Force Account' kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule zinatumika vyema ili kuhakikisha ujenzi bora wa majengo ya shule unakamilika kwa wakati na unatekelezwa kwa kiwango cha hali ya juu.

Aidha, kikao hicho kilifikia tamati kwa Wakuu wa Shule kuweza kutoa maoni yao na kuahidi kuwa watatekeleza yote waliyoagizwa kuyafanya ikiwemo suala zima la usimamizi wa miundombinu ya Shule na Taalumu kwa ujumla.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.