Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mkurugenzi wao Bi. Sipora Liana leo tarehe 15 Septemba, 2018 wameadhimisha Siku ya Usafi Duniani kwa vitendo kwa kufanya usafi katika viwanja vya Karimjee kwa lengo la kuyaweka mazingira ya eneo hilo katika hali ya usafi na ya kuvutia.
Siku ya Usafi Duniani huadhimishwa duniani kote kila Septemba 15 kwa lengo la kuhimiza usafi wa mazingira. Lengo la Tanzania: Kushirikisha watu milioni 1.1 (5% ya idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi) katika kusafisha maeneo yaliyokithiri kwa uchafu Tanzania na kuondoa tani 16,500 za uchafu unaotupwa kinyume cha sheria.
Akiongea mara baada ya zoezi hilo la usafi, Bi. Sipora aliwashukuru watumishi walioshiriki zoezi hilo la kufanya usafi wa mazingira ili kuonyesha mfano kwa jamii na amewataka kuwa mabalozi katika maeneo wanapoishi kwa kutokutupa taka hovyo ili kuweza kuliweka Jiji la Dar es Salaam katika mazingira safi, salama na ya kuvutia.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.