• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Waziri Mkenda awapongeza Watendaji wa NECTA kwa kufanya kazi kwa weledi

Tarehe iliyowekwa: November 30th, 2023

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda ametoa pongezi kwa watendaji wa baraza la mitihani la Tanzania ( NECTA) kwa kufanya kazi kwa weledi pamoja na kusimama madhubuti kwa miaka 50 kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea ikiwa ni pamoja na kupambana na rushwa.

Prof. Mkenda ameyasema hayo Novemba 30, 2023 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam wakati akifungua maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) yaliyoambatana na kauli mbiu isemayo ‘Upimaji wa umahiri kwa Misingi ya haki suluhisho la ajira katika Karne ya 21’

Akiendelea kuzungumza wakati wa maadhimisho hayo Prof. Mkenda amesema “Baraza la Mitihani la Tanzania lilianzishwa rasmi mwaka 1973 na mpaka sasa limetimiza miaka 50 hivyo nipende kuwapongeza watendaji wa NECTA kwa kusimamia vyema baraza hili ndani ya miaka 50 kwani mmeweza kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuhakikisha mnapambana na rushwa   wanafunzi wanafaulu bila udanganyifu hivyo kwakutambua mchango wenu kwenye kuboresha sekta ya Elimu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amezidi kutoa kipaumbele kwenye sekta ya elimu ambapo amehakikisha kila mtoto anapewa fursa ya kusoma hata hivyo katika kutekeleza hayo sisi kama Wizara tumeanza kushirikiana na vyuo vikuu na tutafungua matawi  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mikoa ya Tanga Kagera na Ruvuma ambayo yatakua chachu kwa wanafunzi ambao wanashindwa kusoma Dar es Salaam kwaajili ya umbali na gharama za maisha.”

Sambamba na hayo Prof. Mkenda ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuboresha sekta ya elimu kwani wameanza kujenga Shule za Sekondari za Sayansi za Wasichana kwa kila Mkoa huku wakiendelea kutoa kipaumbele kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa kugawa vifaa wezeshi vya kujifunzia kwa wanafunzi hao kama vitabu vya nukta nundu pia Serikali imejenga Shule Jumuishi kwaajili ya watoto wote wenye mahitaji maalumu hivyo ametoa wito kwa wazazi kutoficha watoto walemavu nyumbani kwani kila mtoto anahaki ya kupata elimu na ukizimgatia elimu kwa sasa ni bure.

Aidha, Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Abdallah Komba amemuhakikishia Mheshimiwa Waziri kufanya kazi kwa ushirikiano na NECTA ili kuhakikisha wanadhibiti udanganyifu na kila mwanafunzi anapimwa katika uimara wake.

Awali akitoa taarifa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Said Mohammed ameeleza kuwa NECTA imekua ikitatua changamoto mbalimbali za wanafunzi kwa kuhakikisha hakuna udanganyifu na kwa sasa suala la kupata vyeti limeboreshwa kwani baada ya matokeo kutoka vyeti vinachukua miezi 3 tu.

Sambamba na hilo Dkt. Mohammed ameeleza kuwa “katika kuadhimisha maadhimisho  hayo baraza litafanya kazi mbalimbali ikiwemo Kupanda miti katika shule za msingi na sekondari nchi nzima, zoezi  lilianza mwezi Oktoba na linatarajia kukamilika mwezi Desemba 2023,Kuendesha mafunzo kwa walimu wa Taaluma kuhusu Utunzi wa maswali yanayopima umahiri na mada zenye changamoto ya ujifunzaji. Baraza liliendesha mafunzo kuanzia tarehe 9 Novemba 2023 hadi tarehe 10 Novemba, 2023 kwa walimu wa Taaluma 180 wa shule za msingi na sekondari ambapo  Walimu hao waliteuliwa katika Halmashauri za Mkoa wa Tanga, Kongamano la Kitaaluma lililofanyika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kuanzia tarehe 27 Novemba, 2023 hadi tarehe 28 Novemba, 2023, Uandishi wa Kitabu cha Historia ya Baraza la Mitihani la Tanzania (1973-2023), Maonesho ya kazi za Baraza la Mitihani la Tanzania na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 30 Novemba, 2023 hadi tarehe 3 Desemba, 2023 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Ujenzi wa Mnara wa Makumbusho utakaozinduliwa tarehe 4 Desemba, 2023 pamoja na Kilele cha Maadhimisho kitakachofanyika tarehe 4 Desemba, 2023 katika Ofisi za baraza hivyo nikuhakikishie mheshimiwa Waziri kazi hizo tumefanya kwa weledi na tunaendelea kufanya bila kusahau majukumu yetu kama baraza ya kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu lengo likiwa ni kupata watendaji bora hapo badae  huku tukihakikisha baraza linafanya kazi kwa  kutekeleza sera ya elimu iliyoboreshwa ili kukuza sekta ya elimu nchini.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.