• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Waziri Mkuu aipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

Tarehe iliyowekwa: May 31st, 2018

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa (Mb) leo tarehe 31 Mei, 2018 amezindua rasmi maonyesho ya Wiki ya Mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni tarehe 5 Juni, 2018.

Akizindua rasmi maonyesho hayo Waziri Mkuu alieleza sababu za kuchagua Jiji la Dar es Salaam katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kitaifa kwa mwaka 2018 kuwa ni pamoja na historia na changamoto nyingi za mazingira zinazolikabili Jiji hili ambalo ni kitivo na kitovu cha shughuli zote za uchumi nchini Tanzania.

Waziri Mkuu ametoa pongezi kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa jitihada inazofanya za kuwawezesha wajasiriamali wadogo kuanzisha viwanda vya nishati mbadala ili kupunguza matumizi makubwa ya nishati ya mkaa ambayo yamesababisha kiasi kikubwa cha misitu yetu kuteketezwa na ametoa wito kwa Halmashauri za Miji, Wilaya, Manispaa na Majiji nchini kuiga jitihada za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kuwawezesha wajasiriamali kuanzisha viwanda vya nishati mbadala.

Aidha Waziri Mkuu ametoa wito kwa Mikoa yote, Taasisi za Serikali na za binafsi kote nchini pamoja na wananchi wote kwa ujumla kuadhimisha siku hii kwa vitendo hususan kwa kufanya shughuli za uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya makazi, maeneo ya mikusanyiko na mjumuiko ili mazingira yawe safi na salama.

Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo ameeleza kuwa kwa mujibu wa Takwimu za hadi kufikia mwaka 2017 zinaonesha kuwa kiasi cha hekta 46,942 za msitu kimekuwa kikiteketezwa kila mwaka na matumizi makubwa yakiwa ni nishati ya mkaa, na inakadiriwa kuwa Jiji la Dar es Salaam linatumia wastani wa tani 500,000 ya mkaa kila mwaka kiasi ambacho kinakadiriwa kuongezeka sana kutokana na ongezeko kubwa la watu kwa kila mwaka.

Mhandisi Ndikilo aliendelea kueleza kwamba Mkoa wa Dar es Salaam unakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira zikiwemo mafuriko, athari za mabadiliko ya Tabianchi zinazosababisha kuongezeka ujazo wa bahari na mawimbi makubwa yanayosababisha kubomoka kingo za bahari.

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira yaliamuliwa mwaka 1972, katika mji wa Stockholm nchini Sweden, kwenye mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa uliohusu Mazingira. Wakati wa mkutano huo Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani, yaani United Nation Environment Programme, UNEP, lilipitishwa tarehe 5 Juni.  Tangu wakati huo, nchi mbalimbali zimekuwa zikiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, tarehe 5 Juni ya kila mwaka, kwa ujumbe maalumu unaotolewa na Umoja wa Mataifa.

Kimataifa maadhimisho haya yana kaulimbiu isemayo “Beat Plastic Pollution”. Kaulimbiu hii inahimiza jamii kuepuka uchafuzi wa Mazingira utokanao na plastiki. Maamuzi ya kupeleka maadhimisho haya nchini India ni kutokana na nchi ya India kuweka juhudi katika kupunguza uchafuzi wa Mazingira utokanao na plastiki kwa kutumia mbadala wa plastiki na kurejeleza taka za plastiki. Aidha, India ni moja ya nchi zilizo mstari wa mbele katika kurejeleza taka za plastiki ukilinganisha na nchi nyingi duniani.

Kitaifa maadhimisho haya yanafanyika jijini Dar es Salaam, Kaulimbiu inayoongoza maadhimisho haya ni “Mkaa Gharama; Tumia Nishati Mbadala”. Kaulimbiu hii inahimiza jamii kupunguza matumizi makubwa ya Nishati ya mkaa ambayo yamesababisha kiasi kikubwa cha misitu yetu kuteketezwa.

Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na wananchi wameshiriki maonyesho hayo na kupata fursa ya kuona, kujifunza na kuwa na uelewa  mkubwa  wa  namna ya kutumia nishati mbadala badala ya kuwa na matumizi makubwa  ya nishati ya mkaa.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.