Na Neema Njau
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Ng’wilabuzu Ludigija leo tarehe 1 Septemba 22 amezindua chanjo ya Polio ya matone awamu ya tatu katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizindua chanjo hiyo Amewapongeza wazazi wote waliojitokeza kwa wingi kuwaleta watoto wenye umri chini ya miaka mitano kupata chanjo hiyo.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewahamasisha wananchi kuwapa ushirikiano watoa huduma za afya wanaopita nyumba kwa nyumba pamoja na vituo vyote vya kutolea huduma za afya ili watoto waweze kupata chanjo na kukingwa dhidi ya ugonjwa wa kupooza ambao hauna tiba.
Naye Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam Dr Elizabeth Nyema ameeleza kuwa Halmashauri imejipanga vizuri kwa zoezi la chanjo ya Polio ya matone kwa kata zote 36 na mitaa 159 ambapo kuna jumla ya wahudumu 1287 wanatoa huduma hii.
Mganga Mkuu ameweza kutembelea Kituo cha Afya Kipawa ambapo ameridhishwa na mwitikio wa utoaji chanjo ya Polio ya Matone ambapo hadi muda aliotembelea kituo hicho watoto 112 walikua tayari wamepatiwa chanjo.
Aidha ameweza kupita kwa baadhi ya watoa huduma nyumba kwa nyumba na kushughudia mwitikio na watoto wakipatiwa chanjo hiyo inayotolewa bure bila malipo.
Zoezi hili la chanjo linafanyika kuanzia leo tarehe 1 hadi 4 Septemba, 2022 .
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.