Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamefanya ziara ya mafunzo ya siku mbili katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Lengo la ziara hiyo ni kubadilishana ujuzi na uzoefu katika usimamizi wa taka ngumu zinazozalishwa jijini Arusha na kuweza kuboresha usimamizi na udhibiti taka ngumu zinazozalishwa jijini Dar es Salaam pamoja na usimamizi wa Dampo ili kuweza kuliweka Jiji la Dar es Salaam katika hali ya usafi.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji pia wamepata fursa ya kubadilishana ujuzi na uzoefu katika usimamizi wa shughuli za utalii pamoja na maegesho jijini Arusha kwa kuzingatia kwamba Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imezindua mpango wa uendelezaji utalii jijini Dar es Salaam kwa lengo la kubadili sura ya Jiji kutoka kuwa njia ya kupita wageni (transit hub) na kuwa kituo cha utalii (tourists destination) na kuongeza muda wa wageni kukaa jijini ili kuongeza mapato ya Jiji.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.