JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mkoani Ubungo

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Jonathan Liana leo tarehe 24 Septemba, 2016 akiwa na wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mkoani cha Ubungo.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatarajia kuboresha miundombinu ya kituo hicho na huduma mbalimbali zinazotolewa katika kituo hicho katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 ili kuweza kutoa huduma bora ya usafirishaji.