JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JIJI LA DAR ES SALAAM

Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Jiji wa robo ya pili, Oktoba-Desemba 2016

Waheshimiwa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutoka katika Manispaa za Kinondoni, Temeke na Kigamboni wakila kiapo tarehe 10 Machi, 2017 mbele ya Mheshimiwa T J Kisoka, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive.

Hafla hiyo ya kuapishwa kwa Waheshimiwa Madiwani ilifuatiwa na mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wa robo ya pili, Oktoba-Desemba, 2016.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam linaundwa na Madiwani ishirini na tano (25) kutoka Manispaa tano (5) za Jiji la Dar es Salaam ambazo ni: Manispaa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni.