Halmashauri ya Jijj la Dar es Salaam kupitia Idara ya Utawala na Utumishi leo Februari 8,2023 wameandaa Semina na kutoa Mafunzo kwa watumishi wanaokaribia kustaafu hivi karibuni, Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam yaliwajumuisha Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Afis Utumishi wa Jiji la Dar es Salaam, Watumishi ambao ni wakufunzi kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, watumishi kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii 'PSSF' pamoja na watumishi kutoka bank ya CRDB.
Akifungua mafunzo hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es-Salaam Bi. Tabu Shaibu amesema, baadhi ya watumishi wamekuwa wanahangaika na kulalama kwa changamoto ya ugumu wa maisha mara baada ya muda wao wa utumishi kuisha na kurudi uraiani kuanza maisha mengine nje na kazi ya utumishi wa Umma, ambapo waliowengi hushindwa kuwa na mipango madhubuti ya baadaye.
Akiendelea kuongea katika mafunzo hayo Bi. Tabu Shaibu ameeleza kuwa, kila mtumishi anawajibu wa kuonesha mchango wake mkubwa muda wote hata baada kutoka kazini, jambo linalotoa taswira nzuri na kuonesha mchango mkubwa kwa jamii, kufanya hivyo kutasababisha kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa kustaafu "Tunachokitaka ni kuwa na mchango mkubwa wa wastaafu katika Halmashauri yetu kwani wengi wanaonekana kuogopa kuanza maisha ya uraiani hivyo ni matumaini yangu mafunzo haya yatakua ni njia ya mafanikio kwa watumishi hao wanaoelekea kustaafu"
Aidha, kwa upande wake Afisa utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dares-Salaam, Bi. Benadeta Mwaikambo amebainisha jumla ya watumishi 91 wanatarajia kustaafu kuanzia mwezi Januari mpaka mwezi Desemba mwaka huu akiongeza kuwa kushindwa kuanzisha miradi ya kujikimu kwa watumishi wanapostaafu kuwa ni changamoto kubwa inayowakabili waliowengi baada ya utumishi wao hivyo ofisi ya utumishi ikaamua kuanziisha mafunzo ya kuwaweka tayari wastaafu hao pindi wanapomaliza kuutumikia Umma nakuona maisha mengine kama maisha ya Utumishi.
“Sisi kama Ofisi ya Utumishi tumeona ni vyema kuanzisha mafunzo haya kwani tumebaini kuwa watumishi wengi wa Umma pindi wanapostaafu wanakosa muelekeo wa maisha kwa kuwa walishazoea maisha ya Utumishi hivyo ni katumaini yangu kwamba mafunzo haya yatawapa mwanga wa kuweza kupambana baada ya maisha ya Utumishi wa Umma hii ndo sababu tumewaletea wakufunzi kutoka chuo cha Utumishi wa Umma pamoja na watumishi kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii PSSF ili waweze kupata elimu itakao wafanya wajiandae vyema na maisha ya ustaafu na kuyaona ni kama maisha ya Utumishi wa Umma.”
Sambamba na hilo Bi. Mwaikambo ameeleza kuwa zoezi hili lililoanza la utoaji wa mafunzo ni endelevu na kila mwaka watakua wanafanya mafunzo hayo ya kuwaandaa wastaafu kukabiliana na changamoto zitakazowakabili pindi wanapomaliza majukumu yao ya kuutumikia Umma.
Akitoa Shukrani zake kwa Ofisi ya Utumishi kwa niaba ya Watumishi wengine wanaotarajia kustaafu hivi karibuni Bwana Nashon ameeleza kuwa Sisi kama watumishi tunaotarajia kuataafu tumejiandaa vyema kupokea mafunzo haya na tunawahakikishia yote tutakayoelekezwa tutayafuata na kuyafanyia kazi ili yaweze kutuongoza baada ya maisha ya kuutumikia Umma.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.