Taasisi ya CRDB Bank Foundation imekabidhi pikipiki 39 na bajaji 6 kwa vikundi sita vya wanawake na vijana jijini Dar es Salaam ukiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa utoaji mikopo jumuishi itokanayo na mapato ya asilimia 10 ya halmashauri za mfano kwa awamu hii ya kwanza.
Hafla ya makabidhiano hayo imeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo aliyeambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya.
Kwa upande wa CRDB Bank Foundation alikuwepo Mkurugenzi Mtendaji, Tullyesther Mwambapa aliyeambatana na Meneja wa Kanda ya Dar es Saalaam, Muhumuliza Buberwa pamoja na wafanyakazi wengine wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation na Benki ya CRDB.
Kupitia ushirikiano huu ambao vijana, wanawake na makundi maalum ya jijini Dar es Salaam wanaendelea kunufaika na fursa hizo, hatua inayowainua kiuchumi na kuchangia ustawi wa jamii kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.