Na: Shalua Mpanda - Mbeya
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunngano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Jamii kuwapa vijana nafasi kwa kuwa ndio nguzo kuu ya maendeleo katika kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Ameyasema hayo jana Oktoba 10,2025 wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Uhindini.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema, katika kutambua hilo, Serikali imetoa kiasi cha shilingi Trilioni 3.5 hadi kufikia mwaka 2024 ukilinganisha na shilingi bilioni 904 kwa mwaka 2021 ili kuwawezesha vijana kiuchumi.
"Vijana wamekuwa nguzo muhimu sana hapa nchini katika uzalishaji hasa katika sekta za teknolojia, kilimo, biashara na michezo, kwa kulitambua hilo ndio maana Serilali imekuwa ikiongeza bajeti kila mwaka ili kuwezesha vijana kiuchumi ". Alisema
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Ridhiwan Kikwete amesema Serikali inatanbua umuhimu wa Vijana na inawekeza kuthamini mchango wao katika kuleta matokeo chanya katika Jamii.
Wiki ya Vijana Kitaifa huadhimishwa kila Mwaka Oktoba 8 hadi 14 kwa kuwakutanisha vijana kutoka Tanzania bara na Visiwani kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, kwa lengo la kujadiliana, kuonesha vipaji, bunifu na kazi wanazofanya.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.