Kamati ya kudhibiti Ukimwi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 10 Mei ,2023 wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli za kilimo na ufugaji zinazofanywa na kikundi cha ‘Upendo Kwa Wote’ kilichopo Chanika Jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa ziara hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Aidan Kwezi amesema “Nipende kuwashukuru sana wanakikundi wa Upendo kwa wote kinachosimamiwa na KONGA (Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Wilaya) kwani wamekua wakifanya vizuri sana hadi kutupelekea Leo hii kuja kukagua miradi Yao japo ni sehemu ya majukumu yetu lakini pia kutambua mchango wao katika kutoa elimu kwa umma juu ya kudhibiti maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI hivyo ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa miradi pamoja na kuhakikisha huduma zote zinazotolewa kwa Waviu zinatekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023 ulioanza Januari hadi Machi 2023."
Aidha Mhe. Kwezi ameendelea kusema “Ziara yetu imekua na mafanikio zaidi kwani kikundi cha Upendo kwa Wote kimekua na mafanikio makubwa sana hivyo niwapongeze watendaji wote kwa ufuatiliaji wa karibu huku tukiwaahidi kutatua changamoto zao ikiwemo fidia ya shamba pamoja na changamoto ya maji kwani tukitekeleza hayo kikundi hicho kitakua ni darasa la watu wengine kujifunza."
Sambamba na Hilo Mhe. Kwezi ametoa wito kwa vikundi vingine vya WAVIU kuiga Mfano wa kikundi cha Upendo kwa wote kwani juhudi zao zilizoonekana ni dira kwa vikundi vingine kujifunza mengi zaidi.
Awali akiwasilisha taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi Katibu wa kikundi cha Upendo kwa wote Bi. Joyce Lyimo ameeleza kuwa Kikundi cha upendo kwa wote kilichoanzishwa mwaka 2015 na kusajiliwa mwaka 2019 kikiwa na wanakikundi 10 ambao ni akina mama WAVIU walioamua kujiunga pamoja kwa lengo la kujiinua kiuchumi kupitia ujasiriamali.
Sambamba na hilo Bi. Joyce ameeleza kuwa “‘Kikundi cha Upendo’ kwa wote kinajishughulisha na shughuli za kilimo, ufugaji, ukaushaji wa matunda, utoaji wa elimu ya ujasiriamali kwa jamii pamoja na kutoa elimu ya VVU na UKIMWI kwa jamii hivyo tunatoka shukrani zetu kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na wajumbe wote wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI kwa kutambua umuhimu wetu hadi kwani mkopo wa asililimia10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri umekuwa msaada mkubwa sana kuwezesha shughuli zetu hivyo tunawaahidi tutaendelea kuhamasisha wananchi wengine kupata elimu zaidi juu ya VVU na Ukimwi huku wakitambua kuwa kuishi na VVU sio mwisho wa maisha.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.