Katika kutekeleza sera ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii Leo Mei 02, 2023 wametoa mafunzo kwa Kamati ya kudhibiti VVU/UKIMWI ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa namna ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Arnatouglou uliopo Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam yaliweza kuhudhuriwa na madiwani ambao ni wajumbe wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ikiongozwa na Naibu Meya wa Jiji, Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na viongozi wote wa baraza la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (KONGA).
Akifungua Mafunzo hayo Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Ojambi Masaburi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI amesema “Ni matumaini yangu mafunzo Haya yatawajengea ninyi Kama Kamati ya kudhibiti UKIMWI uwezo juu ya namna ya kudhibiti UKIMWI katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwani Nina Imani mtashirikiana na wadau mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huo hatarishi na hatimaye kufikia malengo mliyojiwekea.”
Akiwezesha mafunzo hayo maratibu wa VVU/UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (CHAC) Ndg. Barnabas Kisai ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameendelea kutekeleza afua mbalimbali za kudhibiti VVU na UKIMWI kwani Halmashauri kupitia mapato ya ndani imekua ikitenga fedha kiasi cha shilingi milioni 150 kwaajili ya kuhakikisha Jamii inahamashwa zaidi juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI na pia kuhakikisha wale wote walioadhirika na ugonjwa huo kujitokeza kwa wingi ili kuweza kupata huduma kwa karibu zaidi.
Aidha Ndg. Kisai aliweza kutoa maelezo jumla ya uratibu wa shughuli za VVU/UKIMWI katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam huku akiwakumbusha Wajumbe wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI wajibu na majukumu yao katika kuhakikisha wana tekeleza afua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI na pia kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi wa Kata zao juu ya namna ya kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI. “Japo tunawakumbusha majukumu yenu lakini pia tunawashukuru sana Madiwai wa Kamati yetu ya kudhibiti UKIMWI kwa kupambana kuhakikisha Kamati inaendelea na utekelezaji wa afua mbalimbali za VVU na UKIMWI katika Halmashauri yetu." Ameeleza Ndg. Kisai
Naye Mratibu wa kudhibiti VVU/UKIMWI Sekta ya Afya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt. Aisha Zuheri (DACC) ameeleza kuwa “Idadi kubwa ya waadhirika wa ugonjwa wa UKIMWI ni vijana wa kike kuanzia umri wa miaka 15 hadi 24 lakini kutoka na jitihada za kutoa elimu Mara kwa mara katika Kliniki zetu tumeweza kufikia asilimia 102.8 ya kufubaza virusi vya UKIMWI katika Halmashauri yetu.”
Sambamba na hilo Dkt. Aisha ameweza kutoa tofauti kati ya VVU na UKIMWI ambapo ameeleza kuwa VVU ni vimelea vidogo ambayo havionrkani kwa macho huku UKIMWI ikiwa ni mkusanyiko wa magonjwa yanayotokana na kudhoofika kwa nguvu za mwili kujikinga na maradhi hivyo sio kila mwenye VVU ana UKIMWI.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la watu wanahis hi na VVU/UKIMWI (KONGA) Bw. Emmanuel Robert Msinga amesema “Napenda kutoa shukrani zangu kwa madiwani wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kwani wamekua na mchango mkubwa sana katika kuhakikisha sisi kama KONGA tunapambana zaidi hadi tumeweza kuanzisha mashamba mbalimbali pamoja na mifugo mbalimbali hii inadhihirisha kuwa sio kila mwathirika wa Ugonjwa wa UKIMWI hawezi kufanya kazi hivyo niwaombe vijana wengine pamoja na watu wengine wenye maambukizi ya ugonjwa wa Uko wasisite kujitokeza na kuungana nasi bila kuogopa kwani sio kila aliyepata maambukizi ndo mwisho wa maisha.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.