Mafunzo ya uanzishaji na uendeshaji wa Tovuti za Serikali kwa Maofisa Habari na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri na Mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa, Geita, Pwani, Manyara na Dar es Salaam chini ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mjini Dodoma yamefunguliwa Mkoani Dodoma na mgeni rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge.
Akisoma hotuba yake, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge ameeleza kwamba Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao wamesanifu Mfumo wa pamoja utakaosaidia kutengeneza na kusimamia tovuti za Serikali ambazo zitakuwa na kiwango na muonekano mmoja ambao ni rahisi wakati wa kufanya maboresho.
Katibu Tawala ameeleza kuwa lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo Maafisa Habari na TEHAMA ili taarifa zinazohusu Serikali ziweze kuwafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati. Kiongozi wa Habari na Mawasiliano Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma “PS3”, Leah Mwainyekule akitoa maelezo ya mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani “USAID” ujulikanao kwa Kiingereza kama “Public Sector Systems Strengthening” (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara katika maeneo yafuatayo:-
Bi. Leah amefafanua kwamba katika uboreshaji wa mawasiliano kwa umma mradi huo unashirikisha Halmashauri na Mikoa yote ya Tanzania bara kwa kuwapa mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa Tovuti za Serikali maafisa habari na maafisa TEHAMA wa maeneo husika.
Awamu ya kwanza ya mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa Tovuti za Serikali kwa maafisa habari na maafisa TEHAMA ilianza kwa mikoa mitano ya kanda ya ziwa: Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu.
Awamu ya pili ya mafunzo kazi ilianza tarehe 20 Machi, 2017 katika kanda za Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Mbeya, Mtwara na Kigoma. Mfumo wa pamoja wa utengenezaji na usimamizi wa tovuti za Serikali unatarajia kuzinduliwa ngazi ya taifa Machi 27 mwaka huu mjini Dodoma ambapo Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Halmashauri zake 185 zitakuwa zinapatikana katika tovuti kwa majina yao
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.