Na: Shalua Mpanda - Morogoro
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Ssalaam Mhe. Omary Kumbilamoto ameongoza msafara wa Waheshimiwa Madiwani wa Jiji hili kufanya ziara ya mafunzo katika bwawa la kuzalisha na kuhifadhi maji la Kidunda lililopo mkoani Morogoro.
Wakiwa katika ziara hiyo iliyofanyika Mei 30, 2025, Madiwani hao wameweza kujionea shughuli mbalimbali za ujenzi zinazoendelea katika bwawa hilo ambalo mara baada ya kukamilika kwake mwakani litamaliza changamoto ya upatikanaji wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Mhe. Kumbilamoto amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwao kama wawakilishi wa wananchi ambao wana jukumu la kutangaza miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
"Tumekuja huku lengo letu ni moja tu kuona kwa macho yetu mambo haya makubwa yanayoganywa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili na sisi tunaporudi kwa Wananchi tuwe na uhakika na kile tunachokisema". Alisema
Kwa upande wake msimamizi wa Mradi huo, Mhandisi Christian amesema zaidi ya kuzalisha maji bwawa hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji ambayo yatasaidia uendeshaji wa mambo mwingine wa kuzalisha maji wa Ruvu hali ambayo itasaidia upatikanaji wa maji kwa kipindi cha mwaka mzima.
Ongezeko la wakazi katika mkoa wa Dar es salaam na Pwani limesababisha hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo haya kuwa na changamoto ambapo inakadiriwa ifikapo mwaka 2032 idadi ya watu katika maeneo haya kufikia milioni 11 na kuhitaji lita za ujazo zaidi ya bilioni 1 kwa siku,hivyo Serikali inapambana kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inawafikia wananchi kwa asilimia 100.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.