Wajumbe wa Kamati za Huduma za mikopo ngazi ya Kata, Halmashuri na Wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi, weledi na kuzingatia sheria na taratibu za muongozo mpya wa utoaji na usimamizi wa mikopo ya asilimia 10% kwa vikundu vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Wito huo umetolewa leo Octoba 6, 2024 na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Fransisca Makoye kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo hayo ambayo yamefanyika Kwa muda wa siku tatu 3 katika Shule ya Uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo Kibaha Mkoani Pwani.
Bi. Makoye amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Wajumbe hao katika kuhakikisha wanakwenda kutoa elimu na kuwajengea uwezo wanufaika wa mikopo hiyo kwa kutumia fursa za kiuchumi zilizopo kwenye maeneo yao ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kifamilia, kijamii na kiuchumi.
"Mikopo hii ya asilimia 10 inakwenda kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo wadogo ambao hawawezi kukopeshwa na benki kwa sababu ya vipato vyao hivyo niimani Mafunzo haya mtakwenda kuzingatia sheria na kanuni za muongozo mpya wa utoaji mikopo hii." Amesisitiza. Bi Makoye.
Wakati huo huo, Bi. Makoye amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa amerudisha mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kwakua mikopo hiyo itakua chachu ya kuwakwamua Kiuchumi.
Hata hivyo ametoa wito kwa Wananchi kutumia fursa hio kujitokeza katika mafunzo ya utoaji wa elimu ili waweze kuwa na uelewa na hatimaye kutengeneza vikundi na kupata mikopo isiyo na riba itakayo waondoa kwenye wimbi la umaskini.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.