Watumishi wa Halmashauri ya Bagamoyo wamevutiwa na mpangilio wa Soko la Kimataifa la Samaki Feri kwa kutenga maeneo kulingana na shughuli zinazofanyika ili kuhakikisha wanawajibika kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Jiji.
Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Bagamoyo Patrick Amon mapema leo Septemba 17,2025 ameyasema hayo mara baada ya ziara ya mafunzo ndani ya Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambapo amesema kuwa utaratibu huo ni mzuri wa kupangilia soko kwa kutenga Kanda 1-8 na kuweka wasimamizi wenye taaluma mbalimbali kulingana na kanda husika ili kuhakikisha shughuli zote zinafanyika kwa weledi na mapato yanakusanywa.
Pia Amon amesema kuwa mradi wa nishati safi uliopo katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri umewavutia na hivyo wanakwenda kulifanyia kazi kwa kupata wazabuni watakaowezesha kupatikana kwa mradi huo katika Halmashauri yao ya Bagamoyo kwani hivi sasa wakaangaji wa Samaki ndani ya Halmashauri ya Bagamoyo wanatumia mitungi binafsi ya gesi katika kukaangia Samaki .
Pamoja na hayo Amon amezitaka Halmashauri nyingine kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwani inavitu vya kujifunza ambavyo vitasaidia Halmashauri zao hasa katika kuboresha vyanzo vya mapato kwa kupanga vyema fukwe zao hasa kwa Halmashauri zilizo karibu na ufukwe wa bahari ili ziweze kuleta tija .
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.