Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Mei 18, 2024 ameongoza Wananchi wa Jiji la DSM kwenye matembezi na mbio za hiyari za Pugu zenye lengo la kuendeleza Kituo cha Hija Pugu, kuendeleza Nyumba ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere aliyoishi wakati akifundisha shule ya Sekondari Pugu, kuboresha maktaba ya Shule ya Sekondari Pugu pamoja na kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Akiongea baada ya kumalizika kwa mbio hizo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuipunguzia mzigo Serikali wa magonjwa yasiyo ambukizwa.
“Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kupambana na magonjwa hayo, jamii inapaswa kuthamini mazoezi na michezo kwa ujumla. Nimefurahishwa na ushiriki wa makundi mbalimbali kuanzia watoto, vijana na wazee hii yote ni katika kuhakikisha tunakua na jamii yenye afya bora kwaajili ya ujenzi wa Taifa letu. Hongereni Sana kwa kujitoa kwenu." amesema Mhe. Majaliwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amesema michezo ni furaha na huleta amani huku akimshukuru Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa ushiriki wake.
Mbio hizo za Kilomita 2, 5, 10 na 21 ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ya kutenga siku ya jumamosi kama siku ya watu kufanya mazoezi, zilianzia na kumalizika kwenye Viwanja vya Hija vya Kanisa Katoliki, Pugu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.