Na: Shalua Mpanda - Tanga
Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ya mpira wa mkono (Handball) upande wa wanawake imeishushia kipigo cha goli 2-9 timu kutoka Jiji la Mbeya katika mchezo uliofanyika asubuhi ya leo katika viwanja vya shule ya sekondari Usagara.
Kipigo hicho kinaendelea kutoa onyo kwa timu nyingine zinazoshriki mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea mkoani hapa.
Mbeya City katika mchezo huo ilionekana mapema kutoweza kuvumilia 'muziki*wa Dar City ambao walionekana kujiandaa vilivyo na mchezo huo.
Hadi timu zinaenda mapumziko tayari Dar City walikuwa wanaongoza kwa magoli manne dhidi ya mawili ya Mbeya City.
Mchezaji Martha Maurice aliendelea kuwa mwiba mkali kwa Mbeya City baada ya kufunga magoli matano huku Magreth akifunga mawili, Cassiana goli moja na Difina moja.
Leo hii kuna michezo kadhaa itaendelea kupigwa kwenye viwanja mbalimbali katika mashindano haya ya SHIMISEMITA hapa mkoani Tanga ambapo timu ya mpira wa miguu inatarajiwa kushuka dinbani jioni ya leo kupambana na Musoma Dc.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.