Kutekeleza ujenzi wa mradi wa Kimkakati wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Mbezi Luis ambacho kitasaidia katika kuongeza mapato ya Halmashauri pamoja na utoaji wa huduma bora ya usafirishaji wa abiria.
Kusimamia kwa ukaribu na kuboresha usimamizi wa mfumo wa ukusanyaji mapato ya Halmashauri kwa njia za kielektroniki.
Kuboresha miundombinu ya dampo la Pugu Kinyamwezi kwa kujenga choo cha umma, bafu pamoja na ujenzi wa sehemu ya kuoshea magari ili kuimarisha utoaji wa huduma.
Kuandika maandiko ya miradi mbalimbali ya Kimkakati.
Kujenga viwanda vidogo vidogo vitakavyotumiwa na akina mama, vijana na watu wenye ulemavu katika kuendesha shughuli za kiuchumi.
Kupanua wigo wa kukuza na kuendeleza utalii jijini Dar es Salaam kwa kununua gari la kubeba watalii na kujenga kituo cha utamaduni katika eneo la dampo la zamani la Mtoni.
Kuboresha usimamizi na uendeshaji wa Redio ya Halmashauri ya Jiji (City FM Redio) inayopatikana kupitia masafa ya 91.7 FM.
Kujenga na kuboresha maeneo ya mapumziko kwa watoto ikiwa ni pamoja na maeneo ya michezo katika eneo la DRIMP.
Kujenga maduka ya biashara Mwananyamala na DRIMP.
Kuanda andiko la mradi wa ujenzi wa Maktaba na bwalo katika shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa.