Utangulizi
Jiji la Dar es Salaam lipo kati ya Latitudo nyuzi 6 hadi 7 na Longitudo kati 39.45 kwa upande wa Mashariki na nyuzi 39 kwa upande wa Magharibi, Kusini mwa Ikweta na upande wa Magharibi, Kusini na Kaskazini. Jiji linapakana na Mkoa wa Pwani, upande wa Mashariki linapakana na Bahari ya Hindi, ambapo kuna ufukwe wenye urefu wa km. 124 unaoanzia Pemba Mnazi hadi Mbweni.
Jiji la Dar es Salaam lina eneo la ukubwa wa kilomita za Mraba zipatazo 1,800; kati ya hizo, kilomita za mraba 1,350 ni eneo la nchi kavu ikijumuisha visiwa vinane vilivyopo katika eneo la bahari ya Hindi na kilomita za mraba 450 ni eneo la maji ya bahari. Eneo la Jiji la Dar es Salaam ni sawa na asilimia 0.2 ya eneo la nchi nzima ambalo ni kilomita za mraba 881,289.
Hali ya Hewa
Jiji hili lina hali ya hewa ya Joto ya Pwani ya Tropical, likiwa na wastani wa nyuzi joto 25 hadi 33 sentigredi na wastani wa mvua wa mililita 1,000 katika misimu miwili ya vuli ambayo ni miezi ya Oktoba – Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi – Mei. Wakati mwingi Jiji hutawaliwa na pepo zivumazo toka baharini zikitokea Kusini, Mashariki na Kaskazini mwa Bahari ya Hindi.
Idadi ya watu
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 Jiji lina idadi ya watu 4,364,541, ambapo kati yao wanaume ni 2,125,786 na wanawake ni 2,238,755. Aidha, idadi ya watu imekua ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 5.6 kwa mwaka. Wastani wa watu kwa kila kilomita moja ya mraba ilikuwa ni 3,137 na ukubwa wa Kaya ni wastani wa watu 4 kwa Kaya. Kwa ongezeko hilo la watu kwa mwaka, Jiji la Dar es Salaam mwaka 2018 linakadiriwa kuwa na idadi ya watu 6,107,473. Idadi hii ya watu inaongeza msongamano wa watu wanaokadiriwa kuwa 4,383 kwa kila kilometa moja ya mraba.
Historia ya Halmashauri ya Jiji
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa inaliongoza Jiji kutoka mwaka 1961 mpaka mwaka 1972, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizivunja Halmashauri zote nchini na kuwa chini ya Usimamizi wa Serikali Kuu (Madaraka Mikoani)
Serikali Kuu ilizirudisha Serikali za Mitaa Nchini, Chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na. 8 ya mwaka 1982, ambapo Halmashauri ya Jiji ilianza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwaka 1983.
Mwaka 1996 Serikali Kuu iliivunja Halmashauri ya Jiji na kuunda Tume ya Jiji la Dar es Salaam, kwa Tangazo la Serikali Na. 110 na 111 ya tarehe 28 Juni mwaka 1996.
Tume ya Jiji ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka minne, ambapo mwaka 2000 Serikali iliunda mamlaka nne za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya Mwaka 1982, kama ilivyo rekebishwa kwa sheria na. 6 ya mwaka 1999.
Utawala
Kiutawala Jiji limegawanyika katika Halmashauri sita za Serikali za mitaa ambazo ni:
Muundo
Halmashauri ya Jiji inaundwa na Baraza la Madiwani, Idara tano na Vitengo vinne.
Baraza la Madiwani
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam linaundwa na Madiwani 26 kutoka katika Manispaa tano za Jiji la Dar es Salaam na linawakilishwa na Wajumbe wafuatao: Mameya 5, Madiwani 16 na Wabunge 5.
Mstahiki Meya wa Jiji ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Jiji ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa.
Majukumu ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliundwa na kupewa majukumu ya kuratibu na kusimamia shughuli za uendelezaji wa Jiji katika Halmashauri za Manispaa zote tatu. Majukumu hayo ni kwa mujibu wa Sheria za serikali za mitaa (Mamlaka za Miji) Na.8 ya mwaka 1982 kifungu cha 69A kama ilivyorekebishwa na sheria Na.6 ya mwaka 1999.
Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:
Uboreshaji wa Muundo wa Jiji la Dar es Salaam kuwa mamlaka sita umeleta ufanisi mkubwa katika utoaji bora wa huduma kwa jamii kwani madaraka yamesogezwa karibu zaidi na wananchi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.