Na: Aritha Mziray - Tanga
Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imeendelea kutikisa katika michuano ya SHIMISEMITA 2025 baada ya kuichakaza Kinondoni MC katika mchezo wa kikapu (Basketball)
Katika michuano hiyo, Dar city ilipata ushindi wa vikapu (16-2) dhidi ya Kinondoni MC, ikiwa ni ushindi wa kwanza wa kikapu katika michuano hii .
Michezo hiyo inaendelea kwenye Uwanja wa Mkwakwani stadium, Jijini Tanga ambapo Dar City bado inaendelea kuonyesha ukali katika awamu za awali za mashindano.
Timu ya Jiji inasubiria ratiba itakayofata kufahamu itakutana na timu kutoka halmashauri ipi katika mashindano hayo yaliyoanza rasmi leo Agosti 15 hadi 29 mwaka huu ambapo jumla ya halmashauri 141 zinashiriki.
Mashindano hayo yanayoshirikisha halmashauri zote nchini yenye kauli mbiu "Jitokeze Kupiga Kura kwa Maendeleo ya Michezo" yameanza rasmi Agosti 15 na yanatarajiwa kukamilika Agosti 29 mwaka huu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.