Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amezindua Kongamano kubwa la wajasiriamali lenye lengo la kutoa elimu kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii.
Akiongea na wananchi na Wajasiriamali waliojitokeza katika kongamano hilo lililofanyika leo Novemba 11, 2024 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza kuwa Halmshauri ya jiji la Dar es salaam imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 14 kwa ajili ya mikopo kwa makundi ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza mapato katika Nchi.
Sambamba na hilo, Mhe Mpogolo amesema “Ni imani yangu Elimu hii ya mikopo inayotolewa na Halmshauri yetu itawasaidia Wajasiriamali kujua kanuni na sheria za mikopo, pia Wajasiriamali wataweza kusimamia miradi yao vizuri.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar Salaam Elihuruma Mabelya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Aidha Mkurugenzi Mabelya ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ni moja ya Halmashauri 10 za mfano zinazotumia mfumo mpya wa kibenki kutoa mikopo
Kongamano hilo linalofanyika kwa ushirikiano na Taasisi ya AMO, linatarajiwa kufungwa kesho Novemba 12 na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.