Na: Shalua Mpanda
Mkuu wa wilaya IIlala Mhe. Edward Mpogolo amewataka askari wa kike katika majeshi yote wilayani humo kushirikiana ili kuweza kutimiza malengo yao kazini na nje ya kazi.
Ametoa kauli hiyo leo Juni 27,2025 wakati akizungumza na askari wanawake wa Mtandao wa Polisi Wanawake( TPF NET) Mkoa wa Kipolisi Ilala katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.
Mhe. Mpogolo amesema askari wa kike wana majukumu makubwa katika Jamii ikiwa ni pamoja na ulinzi wa raia na mali zao lakini pia kama walezi na walinzi wa familia.
Ameongeza kuwa ili askari hao wawe na nguvu na ya kuweza kufanya mambo makubwa katika jamii wakiwemo kazini na nje ya kazi, ni lazima washirikiane na askari wengine wa kike kutoka majeshi mengine.
'Wito wangu kwa majeshi mengine ni kuona sasa umuhimu wa kuwa na mtandao wa askari wanawake, tutahakikisha tunakaa pamoja na kutafakari namna ya kusaidia askari hawa". Alisema Mkuu huyo wa Wilaya
Kwa upande wake Mkuu wa Mtandao wa Polisi Wanawake mkoa wa kipolisi Ilala,Kamishna Msaidizi Mwandamizi (ASP) Hasina Tawfiq amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupandisha vyeo askari wengi wa kike katika kipindi chake cha uongozi wake.
Aidha, amesema katika kikao hicho cha siku moja kitawawezesha kupata ufahamu wa masuala mbalimbali yakiwemo uwekezaji katika mifuko ya Serikali na hivyo kuwasadia kujikwamua kiuchumi.
Kikao kazi hicho kiliwakutanisha askari wanawake kutoka vikosi vya viwanja vya ndege, Bandari, Marine, Reli na vikosi vingine.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.