Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania kwa kushirikiana na na Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women Leo tarehe 18 Novemba, 2024 limekutana na wadau mbalimbali katika ukumbi wa mdogo wa mikutano Arnatoglou katika hatua ya kufanya tathmini ya kati ya Ripoti ya Maswala ya Jinsia ya Mwaka 2020, ikiwa na lengo la kuangalia uhuishaji wa afua za maswala ya jinsia kwenye mkakati wa V wa afua za VVU na UKIMWI (V)
Akitoa maoni katika tathimini hiyo Mratibu wa uzazi wa mama na mtoto wa Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Moshi Athumani amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya ukatili wa kijinsia na amehusia jamii hasa akina baba majumbani ndio wamekuwa chanzo kikubwa kwa ukatili kwa wanawake na watoto kwani wamekuwa wakiwapiga na kuwanyanyasa Kimwili, kimawazo na kifikra pindi wanapokuwa wameshindwa kufanya jambo lolote, pia mwanamke anapokwenda kliniki na kugundulika kuwa na maambukizi ya Ukimwi wanaume huwa wanawanyanyapaa na wengine kufukuzwa nyumbani
Sambamba na hilo, Bi Moshi ametoa mapendekezo yake na kutoa wito kwa wananchi wote wa jinsia zote za kike na kiume kushiriki katika Elimu ya jinsia na virusi vya ukimwi zinazotolewa na Wataalamu kutoka Serikali, taasisi na Asasi za kidini ili tuweze kutokomeza ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto unaopelekea kuongeza hatari ya kundi hili kuwa kwenye hatari ya kapata maambikizi ya VVU.
Naye Mratibu wa VVU /UKIMWI Sekta ya Afya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (DACC) Dkt. Aisha Zuheri ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika harakati za kuhuisha maswala ya jinsia na UKIMWI, imeanzisha kliniki za vijana rika zinazotoa huduma rafiki ya afya ya uzazi kwa vijana wa makundi yote (Wanaoishi na VVU na Wasio na Maambikizi) lengo likiwa ni kutoa Elimu ya ugonjwa wa Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa , pia kutoa ushauri kwa vijana ili kupunguza hatari ya maambukizi ya VVU, na kusema kuwa Hadi sasa kuna vituo vitano ambavyo vinatoa huduma hiyo.
Kwa Upande wake Mshauri kutoka UN Women Dkt. Patrick Kanyamwenge ameeleza kuwa Tathimini hii lengo lake ni kupata mtazamo, maoni na mapendekezo ya kuboresha utekelezaji wa afua za maswala ya jinsia na kuyauhisha kwenye mkakati wa V wa VVU na UKIMWI ili kuleta ufanisi na kupunguza vitenda vya Kikatili kwenye jamii hasa kwa Akina Mama, mabinti na watoto.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.