Halmashauri ya Jiji la DSM imetenga Bilioni 11 Fedha kutoka asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana , na watu wenye ulemavu.
Hayo ameyabainisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 13, 2024 katika viwanja vya Wikicha vilivyopo Banana Jijini Dar es Salaam wakati akiendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kiwalani, Minazi Mirefu na Kipawa.
Aidha Mhe. Mpogolo ameendelea kusema “Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imetenga Bilioni 11 kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu lengo likiwa nikujikwamua kiuchumi na kukuza uchumi wa Nchi hivyo niwaombe wanufaika wa mikopo hii kuchangamkia fursa na kuacha tabia ya kukopa mikopo yenye riba kubwa inayoumiza”.
Sambamba na hilo, Mhe. Mpogolo amewataka Madiwani na viongozi wa Jiji hilo kuhakikisha mikopo hiyo inapewa kipaumbele kwa wanufaika wenye mahitaji zaidi kama Mama lishe na madereva bodaboda huku akiwataka wataalamu kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoa Elimu ya fedha kwa makundi hayo ili waweze kutumia fedha kwa malengo sahihi ya kukuza biashara zao na kuweza kurejesha mkopo kwa wakati sahihi ili na wengine waweze kunufaika.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.